Showing posts with label Bajeti 2011/2012. Show all posts
Showing posts with label Bajeti 2011/2012. Show all posts

Monday, 27 August 2012

MAPITIO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA NA UJENZI.


MAPITIO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA  NA UJENZI.

Chanzo: Hotuba za Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013.
1.0: SEKTA YA UJENZI:
MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2011/2012
Miradi inayoendelea ni pamoja na Miradi mikubwa ya barabara katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga yenye jumla ya Tshs bilioni 328.235.
Wilaya ya Rombo ina Mradi wa barabara ya;
1.         ROMBO MKUU – TARAKEA (Km 32) wenye thamani ya Tshs bilioni 15.80
2.       Mradi wa barabara ya  MARANGU – ROMBO MKUU – KILACHA – MWIKA (Km 34) Tshs bilioni 25.10
3.       MARANGU – TARAKEA – KAMWANGA/BOMANGOMBE – SANYA JUU (Km 173) na ARUSHA – MOSHI – HOLILI zimetengewa Tshs Milioni 7,854.406
4.       Milioni 488.00 Fedha za Ndani zimetengwa kwa ajili ya kulipia sehemu ya malipo ya mwisho ya Mkandarasi wa barabara ya TARAKEA – ROMBO.
5.       Tshs Milioni 2,146.00 kwa ajili ya kukamilisha Km 6 za lami kwa barabara ya MARANGU – ROMBO MKUU na MWIKA KILACHA (Km 34).
6.       Milioni 2,926.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya Ujenzi wa sehemu ya  barabara ya KAMWANGA – SANYA JUU (Km 75)
7.        Milioni 1,366 kuanza ukarabati wa sehemu ya barabara ya ARUSHA – MOSHI –HOLILI kwa kiwango cha lami.
8.       FEDHA ZA MATENGENEZO NA USIMAMIZI KWA KIPINDI CHA JULAI 2011- JUNI 2012 KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011 ZILIZOPELEKWA KWENYE HALMASHAURI YA ROMBO NI TSHS 428,210,377