Showing posts with label Sensa Tanzania. Show all posts
Showing posts with label Sensa Tanzania. Show all posts

Wednesday, 22 August 2012

SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012: NINI MAANA YA SENSA?

Sensa  ni zoezi la kuhesabu watu wote waliomo nchini, kujua mgawanyiko wa watu hao katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maeneo ya utawala na ukusanyaji wa taarifa nyingine zinazohusiana na watu na makazi yao.

HISTORIA YA SENSA TANZANIA.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603. Sensa ya 2012 itakuwa Sensa ya tano baada ya uhuru.

LENGO KUU LA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012.

  • Kwa ujumla, takwimu za sensa ya watu ni za muhimu sana katika kupanga mipango inayohusiana na uchumi, utawala na huduma mbalimbali zinazohitajika katika kuinua hali ya maisha ya watu kitaifa.
  • Takwimu zitokanazo na Sensa uchangia katika uboreshaji wa maisha ya Watanzania kwa kutoa Takwimu sahihi na zinazoendana na wakati kwa ajili ya kutunga sera, kupanga mipango ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma za jamii, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa program mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya watu. Sense zote ni muhimu lakini Sensa ya mwaka 2012 ina umuhimu wake wa kipekee kwa kuwa itatoa viashiria vingi vitakavyotumika katika kutathimini program za MKUKUTA, MKUZA, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa Tanzania Bara na 2020 kwa Tanzania Zanzibar, Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano wa 2011/12-2015/16 na Malengo ya Milenia ifikapo 2025. Viashiria hivi muhimu nipamoja na idadi ya watu ki makazi, ukubwa wa nguvu kazi, idadi ya vifo na vifo vinavyotokana na uzazi, wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania, viwango vya uzazi, idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika na idadi ya watoto walioandikishwa shule. Viashiria vingine ni pamoja na idadi ya kaya zinazoshujishughulusha na kilimo, ufugaji na uvuvi.