Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo juzi saa 2:00 usiku katika eneo hilo.
Aliwataja waliofariki kuwa ni Sophia Christopher
(18), Ashasen Emanuel (30), Amedeus Kweka (28) wakazi wa Mererani,
wengine ni Adam Thegi mkazi wa Musoma na Hatib Athuman (40) mkazi wa
Majengo Arusha.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, waliojeruhiwa
ni Teresia John (35) Wahida Idd (28), Jerad Mtimeili (31) na Linda Mlay
(22) wakazi wa Mererani Manyara.
Makunga ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo, alisema gari aina ya Landrover
Volkswagen lililokuwa likiendeshwa na dereva Amedeus Kweka (28)
likitokea kituo cha mafuta cha Kodil liliingia barabarani huku gari
ikiwaka taa moja.
Alisema dereva huyo aliingia barabarani akiwa
kwenye mwendo kasi na kugongana na gari aina ya Mistubish Canter
likiendeshwa na Francicy Mkongo (37) mkazi wa USA jijini Arusha na
kusababisha ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robart Boaz amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni mwendo kasipamoja na dereva kuendesha gari likiwa halina taa
wakati wa usiku.
www.mwananchi.co.tz
www.mwananchi.co.tz