Wednesday 29 August 2012

Changamoto za Maendeleo Wilaya ya Rombo

Sehemu ya Stendi ya Mkuu 

Marekebisho ya Kiwanda cha zamani eneo la Huruma - Mkuu

majengo ya iliyokuwa Rombo dalta - Mkuu


Barabara karibu na Ofisi za TANESCO Mkuu

Uwekezaji wa majengo ya Biashara katika eneo la Tarakea)
Miundombinu ya Barabara, Uwekezaji, Huduma za Jamii pamoja na Kuendeleza Miradi iliyopo ni changamoto kubwa katika kuhakikisha Rombo inakuwa na Maendeleo endelevu na Wananchi wanakuwa sehemu ya Maendeleo hayo kwa kuongezeka kwa Huduma na Kipato. (Pichani: Sehemu ya Stendi ya Mkuu - Wilayani, majengo ya iliyokuwa Rombo dalta - Mkuu, Marekebisho ya Kiwanda cha zamani eneo la Huruma - Mkuu, Barabara karibu na Ofisi za TANESCO Mkuu na uwekezaji wa majengo ya Biashara katika eneo la Tarakea)

KUTOKA TSAVO HADI ROMBO: Safari ya Tembo kila Mwaka

Sehemu ya Mbuga ya Wanyama ya TSAVO kama inavyoonekana katika eneo karibu na MWATATE Nchini Kenya. Wanyama hasa Tembo wamekuwa wakivamia maeneo ya Wilaya ya Rombo kutoka Mbuga ya Wanyama ya Tsavo. Juhudi za dhati zinahitajika kudhibiti wanayama hawa kwani Kifuta machozi kinachotolewa na Serikali kwa uharibifu wa Mazao, kuuawa kwa wanyama wanaofugwa au watu kupoteza maisha hakitoshi.

WAHAMIAJI HARAMU

BANGO LA MAMLAKA YA MJI WA TAVETA:
Mji wa Taveta Nchini Kenya unaopakana na Wilaya ya ROMBO na Milima ya Upare unatajwa kuwa mojawapo ya Njia kuu za kupitishia Wahamiaji Haramu kuingia Tanzania.

VYANZO VYA MAPATO YA SERIKALI ZA MITAA (HALMASHAURI YA ROMBO)


MAPATO YA SERIKALI ZA MITAA

Serikali za Mitaa zina Mamlaka ya kukusanya aina Fulani ya Mapato kutokana na Kodi, levies na fees. Serikali za Mitaa huweka Sera zao za Mapato kulingana na mipaka ya Serikali Kuu. Hubakisha Mapato haya na kuyatumia kama sehemu za Bajeti zao – Mapato haya sio sehemu ya Mapato ya Serikali Kuu. Kodi, levies, fees na Vyanzo vya Mapato ambavyo Serikali za Mitaa zina Mamlaka ya kukusanya  zimewekwa kwa mujibu wa Local Government Finances Act kama ifuatavyo:

A. Taxes on Property

i. Property rates.

B. Taxes on Goods and Services

  1. Crop cess (maximum 5% of farm gate price)
  2. Forest produce cess

C. Taxes on Specific Services

i.       Guest house levy

D. Business and Professional Licenses

  1. Commercial fishing license fees
  2. Intoxicating liquor license fee
  3. Private health facility license fee
  4. Taxi license fee
  5. Plying permit fees
  6. Other business licenses fees

E. Motor Vehicles, Other Equipment and Ferry Licenses

  1. Vehicle license fees
  2. Fishing vessel license fees

F. Other Taxes on the Use of Goods, Permission to Use Goods

  1. Forest produce license fees
  2. Building materials extraction license fee
  3. Hunting licenses fees
  4. Muzzle loading guns license fees
  5. Scaffolding / Hoarding permit fees

G. Turnover Taxes

i.       Service levy

H. Entrepreneurial and Property Income

  1. Dividends
  2. Other Domestic Property Income
  3. Interest
  4. Land rent

I. Administrative Fees and Charges

  1. Market stalls / slabs dues
  2. Magulio fees
  3. Auction mart fees
  4. Meat inspection charges
  5. Land survey service fee
  6. Building permit fee
  7. Permit fees for billboards, posters or hoarding
  8. Tender fee
  9. Abattoir slaughter service fee
  10. Artificial insemination service fee
  11. Livestock dipping service fee
  12. Livestock market fee
  13. Fish landing facilities fee
  14. Fish auction fee
  15. Health facility user charges
  16. Clean water service fee
  17. Refuse collection service fee
  18. Cesspit emptying service fee
  19. Clearing of blocked drains service fee
  20. Revenue from sale of building plans
  21. Building valuation service fee
  22. Central bus stand fees
  23. Sale of seedlings
  24. Insurance commission service fee
  25. Revenue from renting of houses
  26. Revenue from renting of assets
  27. Parking fees

J. Fines, Penalties and Forfeitures

  1. Stray animals penalty
  2. Share of fines imposed by Magistrates Court
  3. Other fines and penalties
Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya ROMBO hazipaswi kutoza taxes, levies au fees ambazo hazipo katika orodha hii.

Monday 27 August 2012

BIASHARA YA FEDHA HARAMU (MONEY LAUNDERING)

Biashara ya Fedha Haramu (Money Laundering) ni Nini?

Biashara ya Fedha Haramu ni shughuli au vitendo vyenye lengo la kuficha ukweli au asili ya fedha au mali iliyotokana na uhalifu.

MAPITIO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA NA UJENZI.


MAPITIO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA  NA UJENZI.

Chanzo: Hotuba za Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013.
1.0: SEKTA YA UJENZI:
MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2011/2012
Miradi inayoendelea ni pamoja na Miradi mikubwa ya barabara katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga yenye jumla ya Tshs bilioni 328.235.
Wilaya ya Rombo ina Mradi wa barabara ya;
1.         ROMBO MKUU – TARAKEA (Km 32) wenye thamani ya Tshs bilioni 15.80
2.       Mradi wa barabara ya  MARANGU – ROMBO MKUU – KILACHA – MWIKA (Km 34) Tshs bilioni 25.10
3.       MARANGU – TARAKEA – KAMWANGA/BOMANGOMBE – SANYA JUU (Km 173) na ARUSHA – MOSHI – HOLILI zimetengewa Tshs Milioni 7,854.406
4.       Milioni 488.00 Fedha za Ndani zimetengwa kwa ajili ya kulipia sehemu ya malipo ya mwisho ya Mkandarasi wa barabara ya TARAKEA – ROMBO.
5.       Tshs Milioni 2,146.00 kwa ajili ya kukamilisha Km 6 za lami kwa barabara ya MARANGU – ROMBO MKUU na MWIKA KILACHA (Km 34).
6.       Milioni 2,926.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya Ujenzi wa sehemu ya  barabara ya KAMWANGA – SANYA JUU (Km 75)
7.        Milioni 1,366 kuanza ukarabati wa sehemu ya barabara ya ARUSHA – MOSHI –HOLILI kwa kiwango cha lami.
8.       FEDHA ZA MATENGENEZO NA USIMAMIZI KWA KIPINDI CHA JULAI 2011- JUNI 2012 KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011 ZILIZOPELEKWA KWENYE HALMASHAURI YA ROMBO NI TSHS 428,210,377


Friday 24 August 2012

Barabara ya Rongai - Kamwanga


Mramba azidi kumkandamiza Mkapa mahakamani


Thursday, 23 August 2012 20:19 (Chanzo: Gazeti la Mwananchi)

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha Basil Mramba, jana aliendelea kumkandamiza aliyekuwa bosi wake na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akimhusisha moja kwa moja na kutolewa kwa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers.

Mramba aliyaeleza hayo jana wakati akijitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni na kwamba alitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo ili kutekeleza matakwa ya mkataba.

Alidai kuwa kifungu cha 4.3.1  kilichopo kwenye  mkataba huo ulioingiwa kati ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Alex Stewart Government Business Assayers kinasema malipo yoyote  yatakayolipwa na mkataba huo hayatotozwa kodi.
“Mimi nilichofanya ni kutekeleza  matakwa ya mkataba huu kwa sababu Waziri wa Fedha  pekee ndiye mwenye mamlaka  ya kutekeleza mkataba huo,” alidai Mramba.

Wednesday 22 August 2012

SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012: NINI MAANA YA SENSA?

Sensa  ni zoezi la kuhesabu watu wote waliomo nchini, kujua mgawanyiko wa watu hao katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maeneo ya utawala na ukusanyaji wa taarifa nyingine zinazohusiana na watu na makazi yao.

HISTORIA YA SENSA TANZANIA.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603. Sensa ya 2012 itakuwa Sensa ya tano baada ya uhuru.

LENGO KUU LA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012.

  • Kwa ujumla, takwimu za sensa ya watu ni za muhimu sana katika kupanga mipango inayohusiana na uchumi, utawala na huduma mbalimbali zinazohitajika katika kuinua hali ya maisha ya watu kitaifa.
  • Takwimu zitokanazo na Sensa uchangia katika uboreshaji wa maisha ya Watanzania kwa kutoa Takwimu sahihi na zinazoendana na wakati kwa ajili ya kutunga sera, kupanga mipango ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma za jamii, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa program mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya watu. Sense zote ni muhimu lakini Sensa ya mwaka 2012 ina umuhimu wake wa kipekee kwa kuwa itatoa viashiria vingi vitakavyotumika katika kutathimini program za MKUKUTA, MKUZA, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa Tanzania Bara na 2020 kwa Tanzania Zanzibar, Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano wa 2011/12-2015/16 na Malengo ya Milenia ifikapo 2025. Viashiria hivi muhimu nipamoja na idadi ya watu ki makazi, ukubwa wa nguvu kazi, idadi ya vifo na vifo vinavyotokana na uzazi, wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania, viwango vya uzazi, idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika na idadi ya watoto walioandikishwa shule. Viashiria vingine ni pamoja na idadi ya kaya zinazoshujishughulusha na kilimo, ufugaji na uvuvi.

Saturday 4 August 2012

Lengo

DIRA

  • Kuwa na Mtandao wa Wakazi wa Rombo unaolenga kuongoza, kushiriki, kushawishi maamuzi na Maendeleo ya Rombo kwenye nyanja mbalimbali.

DHANA

  • Kuwa na Mtandao mpana wenye kujumuisha Wananchi wa Kada zote utakaokuwa na ushawishi katika Sera na Mipango ya Maendeleo ya Wilaya ya Rombo.
  • To reveal Rombo to ideas, analyses and Challenges toward Sustainable development and Reform
  • Expose, Debate and Assess Rombo's growth potentials and limitations.
  • To provide a forum/platform for discussion for a consistent and dedicated development and reform agenda towards a prosperous, Democratic and a Human right conscious Rombo District.
  • Kutafuta, kujadili, kushawishi na Kusambaza Habari zinazohusu  wilaya ya Rombo.