Tuesday 16 July 2013

Mengi: Waliokamatwa na unga ni chambo

MWENYEKITI Mtendaji wa Kampeni za IPP Media, Regnald Mengi amejitosa katika sakata la wasichana waliokutwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam jana, Mengi alidai kuwa wasichana waliokamatwa na dawa hizo wanatumika kama chambo kwani wapo vigogo waliowatuma kufanya shughuli hiyo.
Hivi karibuni wasichana wawili raia wa Tanzania walikamatwa Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya sh. bilioni 6.8 na kwamba walipitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mengi alibainisha kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya inakwama kutokana na vitendo vya rushwa. Alisema rushwa imekuwa chanzo kikubwa cha watu kujihusisha na biashara ya dawa hizo na hivyo kuleta matatizo kwa vijana.   Alisema watu wengi ambao wanajikita katika rushwa ndiyo wanaojiingiza katika biashara hiyo kutokana na kuwa na fedha nyingi. Kutokana na hali hiyo, alisema wananchi wasipokuwa makini wapokea rushwa ndiyo watakuwa watawala wa nchi.
 (Nyendo Mohamed wa JAMBO LEO - www.jamboconcepts.com)

No comments:

Post a Comment