Saturday, 10 November 2012

Mapambano dhidi ya Uvamizi wa Ndovu kutoka Tsavo

Serikali za Tanzania na Kenya leo zimekubaliana kuunda Kamati ya pamoja ikiwa ni juhudi za kutafuta njia za kukabiliana na Ndovu ambao huingia Wilaya ya Rombo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mashamba. kwa muda mrefu wanyama hawa wamekuwa wakihamia sehemu za Wilaya ya Rombo kutafuta malisho hasa kipindi cha kiangazi. kikao hiki cha pamoja kimefanyika wilayani Rombo na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote wakiwemo Mhe. Lazaro Nyalandu na Mhe. Mideye pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Taveta. Aidha Waziri Nyalandu ameahidi kupeleka Askari wa Wanyamapori kwa ajili ya Operesheni maalum.

No comments:

Post a Comment