Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ametumia Madaraka aliyopewa chini ya Kifungu cha 173 (C) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Kifungu cha 78 (C) cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) sura ya 288. Waziri ameziagiza Halmashauri zote Tanzania bara kuweka utaratibu wa Wenyeviti wa Kamati za Maendeleo za Kata (Diwani) kuwasilisha Taarifa za Utekelezaji za Kata na kuweka utaratibu wa Wajumbe wa Halmashauri kuwauliza Wakurugenzi wa Halmashauri na Wenyeviti/Mameya wa Halmashauri Maswali ya papo kwa papo. Taarifa zitakazowasilishwa ni zile ambazo zinahusu pamoja na mambo mengine
- Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo - ujenzi wa Madarasa, nyumba za walimu, Maabara n.k
- Maendeleo ya Elimu - uandikishwaji watoto, utoro, ukauzi, mimba,ufundishaji n.k
- ustawi wa jamii - majanga, magonjwa, vizazi na vifo n.k
- shughuli za kiuchumi - upatikanaji wa wataalam, pembejeo za kilimo, mifugo na uvuvi n.k
- uimarishaji wa dhana ya uzalendo na utaifa - vikundi vya vijana, mafunzo ya jeshi la Mgambo n.k
- Taarifa za Mapokeo ya Fedha na Matumiz yake
Utaratibu huu utasaidia kutoa mwanga katika nyanja mbalimbali ikiwemo
- Uendeshaji wa jumla wa Halmashauri
- Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
- Mipango mkakati ya Halmashauri kuwaondolea wananchi umaskini
- usimamizi na Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka husika
- Uhifadhi wa Mazingira
- Usalama wa Chakula, usalama wa raia na mali zao
- Utawala bora
No comments:
Post a Comment