Thursday, 11 April 2013

USHAURI WA MWINYI

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka Watanzania kusimamia imani zao na kuacha kubughudhiana kwenye masuala ya kuchinja wanyama.
Akizungumza kwenye Kongamano la Utamaduni wa Kiislamu katika nchi za Afrika Mashariki lililofanyika Dar es Salaam jana, Mzee Mwinyi alisema kila mmoja anapaswa kufuata misingi ya dini yake na kutii sheria bila ya kumkwaza mtu mwingine, jambo ambalo litadumisha mshikamano wa Taifa.

No comments:

Post a Comment