Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amekemea vikali vurugu
zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya
Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati
wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa,
Rais Kikwete alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na
kuchukuliwa hatua kali.
Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana
mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote... “Hivi
watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze
basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,”
alihoji kwa ukali Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka
wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo...
“Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani,
tutayakata.” (www.mwananchi.co.tz)
No comments:
Post a Comment