MAPITIO
YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA
HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA
NA UJENZI.
Chanzo:
Hotuba za Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013.
MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2011/2012
Miradi inayoendelea ni pamoja na Miradi mikubwa ya barabara katika
mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga yenye jumla ya Tshs
bilioni 328.235.
Wilaya ya Rombo ina Mradi wa barabara ya;
1.
ROMBO MKUU –
TARAKEA (Km 32) wenye thamani ya Tshs bilioni 15.80
2.
Mradi wa barabara ya MARANGU – ROMBO MKUU – KILACHA –
MWIKA (Km 34) Tshs bilioni 25.10
3.
MARANGU –
TARAKEA – KAMWANGA/BOMANGOMBE – SANYA JUU (Km 173) na ARUSHA – MOSHI – HOLILI zimetengewa
Tshs Milioni 7,854.406
4.
Milioni
488.00 Fedha za Ndani zimetengwa kwa ajili ya kulipia sehemu ya malipo
ya mwisho ya Mkandarasi wa barabara ya TARAKEA – ROMBO.
5.
Tshs Milioni 2,146.00 kwa ajili ya kukamilisha Km
6 za lami kwa barabara ya MARANGU – ROMBO MKUU na MWIKA KILACHA (Km 34).
6.
Milioni 2,926.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza
maandalizi ya Ujenzi wa sehemu ya
barabara ya KAMWANGA – SANYA JUU (Km 75)
7.
Milioni 1,366 kuanza ukarabati wa sehemu ya
barabara ya ARUSHA – MOSHI –HOLILI kwa kiwango cha lami.
8.
FEDHA ZA MATENGENEZO NA USIMAMIZI KWA KIPINDI CHA
JULAI 2011- JUNI 2012 KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011 ZILIZOPELEKWA KWENYE HALMASHAURI YA ROMBO NI TSHS 428,210,377