Monday 27 August 2012

MAPITIO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA NA UJENZI.


MAPITIO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA  NA UJENZI.

Chanzo: Hotuba za Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013.
1.0: SEKTA YA UJENZI:
MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2011/2012
Miradi inayoendelea ni pamoja na Miradi mikubwa ya barabara katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga yenye jumla ya Tshs bilioni 328.235.
Wilaya ya Rombo ina Mradi wa barabara ya;
1.         ROMBO MKUU – TARAKEA (Km 32) wenye thamani ya Tshs bilioni 15.80
2.       Mradi wa barabara ya  MARANGU – ROMBO MKUU – KILACHA – MWIKA (Km 34) Tshs bilioni 25.10
3.       MARANGU – TARAKEA – KAMWANGA/BOMANGOMBE – SANYA JUU (Km 173) na ARUSHA – MOSHI – HOLILI zimetengewa Tshs Milioni 7,854.406
4.       Milioni 488.00 Fedha za Ndani zimetengwa kwa ajili ya kulipia sehemu ya malipo ya mwisho ya Mkandarasi wa barabara ya TARAKEA – ROMBO.
5.       Tshs Milioni 2,146.00 kwa ajili ya kukamilisha Km 6 za lami kwa barabara ya MARANGU – ROMBO MKUU na MWIKA KILACHA (Km 34).
6.       Milioni 2,926.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya Ujenzi wa sehemu ya  barabara ya KAMWANGA – SANYA JUU (Km 75)
7.        Milioni 1,366 kuanza ukarabati wa sehemu ya barabara ya ARUSHA – MOSHI –HOLILI kwa kiwango cha lami.
8.       FEDHA ZA MATENGENEZO NA USIMAMIZI KWA KIPINDI CHA JULAI 2011- JUNI 2012 KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011 ZILIZOPELEKWA KWENYE HALMASHAURI YA ROMBO NI TSHS 428,210,377


2.0: SEKTA YA MAJI:
Mpango wa Utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ulihusu kujenga Miradi ya Maji kwenye vijiji 10  kwa kila Halmashauri, kujenga uwezo kwa watekelezaji wa program, kuhamasisha wananchi kuhusu usafi binafsi na usafi wa mazingira,kusimamia na kufuatilia miradi ya maji. Serikali ilianza kutekeleza program kwa ujenzi na ukarabati wa miradi midogo yenye kuleta matokeo ya haraka (quick wins)  Hadi kufikia Juni 2012, Halmashauri ya ROMBO ilikuwa katika hatua mbalimbali za kuanza Ujenzi.
·        Wakala  (DDCA) alichimba kisima kimoja kwa mwaka 2011/12 katika Halmashauri ya ROMBO
·        Halmashauri ya ROMBO kwa sasa imeanza kuchima visima ambapo visima 9 vimepangwa kuchimbwa, 5 vimechimwa na 4 vina maji. ROMBO katika mwaka 2011/12 ilitumiwa jumla ya Tshs 855,222,668 kwa mchanganuo ufuatao:
ü      Miundombinu ……………………………………………. Tshs 784,574,668
ü      Kujenga  Uwezo ………………………………………… Tshs 70,648.000
·        FEDHA ZA MFUKO WA PAMOJA WA PROGRAMU YA SEKTA YA MAJI ZILIZOTENGWA
Halmashauri ya ROMBO ilitengewa Tshs 443,158,000
·        TANAPA  ndio TAASISI  pekee iliyochangia katika utekelezaji wa Miradi ya maji katika vijiji vya Rombo
·        Mamlaka pekee ya maji iliyopo ndani ya wilaya ya Rombo ni Mamlaka Ndogo ya Maji ya  MKUU ROMBO.

No comments:

Post a Comment