Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier
Daudi amesema ofisi yake hivi sasa itakuwa ikitoa ratiba ya usaili
mapema kila mara ili kuwawezesha wasailiwa kuwa na muda wa kutosha
kujiandaa kabla ya kwenda kwenye usaili husika.
Amesema hayo leo wakati akiongea na mwandishi wa habari ofisini kwake
alipokuwa akitoa ratiba ya usaili kwa mwezi Septemba, 2012 pamoja na
tangazo la kuita kazini waombaji waliofaulu usaili uliopita. Aliongeza
kuwa ili msailiwa aweze kufanya vizuri katika usaili pamoja na vigezo
vya kitaaluma alivyonavyo bado anatakiwa kujiandaa vyema na kujiamini
anapojibu maswali wakati anapokuwa kwenye usaili.
Daudi amesema hivi
sasa dunia imekuwa ya utandawazi na fursa za ajira ni za ushindani
zaidi, maana wahitimu hivi sasa ni wengi na hawana ajira hivyo ni vyema
kwa wahitimu wanapoomba nafasi za kazi na kuitwa kwenye usaili wawe
wamejiandaa vya kutosha ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata
ajira.
Katibu, amesema kwa mwezi Oktoba, 2012 usaili utafanyika
takriban katika mikoa yote ya Tanzania Bara ambapo utahusisha kada
zifuatazo Maafisa Tarafa daraja la II, Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la
II , Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la III, Afisa Mtendaji wa Kijiji
Daraja la II, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III, Afisa Mtendaji
Mtaa II, Afisa Mtendaji Mtaa III, Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II,
Mpishi Daraja la II, Afisa Utamaduni Msaidizi, Mtakwimu Msaidizi, Dereva
Daraja la II, Mhudumu wa Jikoni/ Mess Daraja la II, Mlezi wa Mtoto
Msaidizi, Operata wa Kompyuta Msaidizi, Msaidizi Misitu Daraja La II,
Msaidizi wa Ofisi, Msaidizi Ustawi wa Jamii Daraja la II, Maendeleo ya
Jamii Msaidizi Daraja la II, Mpokezi, Katibu Mahsusi Daraja la III na
Mlinzi
Amesema kwa maelezo zaidi ya nafasi hizo na wapi usaili
utafanyika ni vyema waombaji wakaperuzi tovuti ya Sekretarieti ya Ajira
pamoja na tovuti za Taasisi husika na kufungua tangazo la kuitwa kwenye
usaili ili kuiona ratiba nzima ya tarehe ya mchujo na usaili kama
zinavyoonekana katika tangazo lenye orodha ya majina ya kuitwa kwenye
usaili.
Aidha, amesisitiza ni muhimu kwa waombaji kuzingatia masharti
ya tangazo pindi wanapoenda kwenye usaili kwani ni njia mojawapo ya
kujua msailiwa amejiandaa kwa kiasi gani.
Wakati huohuo, Katibu
amewataka waombaji wa nafasi za kazi waliofanya usaili kuanzia tarehe 7
hadi 31Agosti, 2012 katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Biashara (CBE), Taasisi ya
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo cha Maji (WDMI), Chuo cha Mipango
Dodoma (IRDP), Chuo cha Serikali za Mitaa- Hombolo, COASCO, Tume ya Vyuo
Vikuu (TCU), Tume ya Mionzi (TAEC), Taasisi ya Utafiti wa Samaki
(TAFIRI), Wakala wa Mbegu (TOSCI), Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TASUBA) kuangalia majina yao katika tovuti ya Sekretarieti ya
Ajira pamoja na taasisi husika ili kujua waliofaulu.
Amesema kwa
waliofaulu usaili wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao
umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti
halisi (Originals) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili
vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Aidha, barua za
kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao za posta.
Alimalizia
kwa kusema kuwa, kwa wale ambao hawataona majina yao katika tangazo
husika watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuendelea
kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
Kuongoza, Kushiriki, Kushawishi Maamuzi na Maendeleo ya Rombo
Monday, 31 December 2012
Saturday, 15 December 2012
SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA UWAJIBIKAJI KATIKA SERIKALI ZA MITAA
Serikali ya Tanzania katika kuendelea kutekeleza Programu ya Uboreshaji wa Serikali za Mitaa inakusudia kuimarisha mifumo ya uwazi na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya Serikali za Mitaa.
Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ametumia Madaraka aliyopewa chini ya Kifungu cha 173 (C) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Kifungu cha 78 (C) cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) sura ya 288. Waziri ameziagiza Halmashauri zote Tanzania bara kuweka utaratibu wa Wenyeviti wa Kamati za Maendeleo za Kata (Diwani) kuwasilisha Taarifa za Utekelezaji za Kata na kuweka utaratibu wa Wajumbe wa Halmashauri kuwauliza Wakurugenzi wa Halmashauri na Wenyeviti/Mameya wa Halmashauri Maswali ya papo kwa papo. Taarifa zitakazowasilishwa ni zile ambazo zinahusu pamoja na mambo mengine
Utaratibu huu utasaidia kutoa mwanga katika nyanja mbalimbali ikiwemo
Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ametumia Madaraka aliyopewa chini ya Kifungu cha 173 (C) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Kifungu cha 78 (C) cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) sura ya 288. Waziri ameziagiza Halmashauri zote Tanzania bara kuweka utaratibu wa Wenyeviti wa Kamati za Maendeleo za Kata (Diwani) kuwasilisha Taarifa za Utekelezaji za Kata na kuweka utaratibu wa Wajumbe wa Halmashauri kuwauliza Wakurugenzi wa Halmashauri na Wenyeviti/Mameya wa Halmashauri Maswali ya papo kwa papo. Taarifa zitakazowasilishwa ni zile ambazo zinahusu pamoja na mambo mengine
- Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo - ujenzi wa Madarasa, nyumba za walimu, Maabara n.k
- Maendeleo ya Elimu - uandikishwaji watoto, utoro, ukauzi, mimba,ufundishaji n.k
- ustawi wa jamii - majanga, magonjwa, vizazi na vifo n.k
- shughuli za kiuchumi - upatikanaji wa wataalam, pembejeo za kilimo, mifugo na uvuvi n.k
- uimarishaji wa dhana ya uzalendo na utaifa - vikundi vya vijana, mafunzo ya jeshi la Mgambo n.k
- Taarifa za Mapokeo ya Fedha na Matumiz yake
Utaratibu huu utasaidia kutoa mwanga katika nyanja mbalimbali ikiwemo
- Uendeshaji wa jumla wa Halmashauri
- Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
- Mipango mkakati ya Halmashauri kuwaondolea wananchi umaskini
- usimamizi na Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka husika
- Uhifadhi wa Mazingira
- Usalama wa Chakula, usalama wa raia na mali zao
- Utawala bora
Saturday, 10 November 2012
Mapambano dhidi ya Uvamizi wa Ndovu kutoka Tsavo
Serikali za Tanzania na Kenya leo zimekubaliana kuunda Kamati ya pamoja ikiwa ni juhudi za kutafuta njia za kukabiliana na Ndovu ambao huingia Wilaya ya Rombo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mashamba. kwa muda mrefu wanyama hawa wamekuwa wakihamia sehemu za Wilaya ya Rombo kutafuta malisho hasa kipindi cha kiangazi. kikao hiki cha pamoja kimefanyika wilayani Rombo na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote wakiwemo Mhe. Lazaro Nyalandu na Mhe. Mideye pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Taveta. Aidha Waziri Nyalandu ameahidi kupeleka Askari wa Wanyamapori kwa ajili ya Operesheni maalum.
Wednesday, 29 August 2012
Changamoto za Maendeleo Wilaya ya Rombo
Sehemu ya Stendi ya Mkuu |
Marekebisho ya Kiwanda cha zamani eneo la Huruma - Mkuu |
majengo ya iliyokuwa Rombo dalta - Mkuu |
Barabara karibu na Ofisi za TANESCO Mkuu |
Uwekezaji wa majengo ya Biashara katika eneo la Tarakea) |
Labels:
Mkuu Rombo,
Rombo Dalta,
Stendi Mkuu
Location:
Mkuu, Tanzania
KUTOKA TSAVO HADI ROMBO: Safari ya Tembo kila Mwaka
Sehemu ya Mbuga ya Wanyama ya TSAVO kama inavyoonekana katika eneo karibu na MWATATE Nchini Kenya. Wanyama hasa Tembo wamekuwa wakivamia maeneo ya Wilaya ya Rombo kutoka Mbuga ya Wanyama ya Tsavo. Juhudi za dhati zinahitajika kudhibiti wanayama hawa kwani Kifuta machozi kinachotolewa na Serikali kwa uharibifu wa Mazao, kuuawa kwa wanyama wanaofugwa au watu kupoteza maisha hakitoshi.
WAHAMIAJI HARAMU
BANGO LA MAMLAKA YA MJI WA TAVETA:
Mji wa Taveta Nchini Kenya unaopakana na Wilaya ya ROMBO na Milima ya Upare unatajwa kuwa mojawapo ya Njia kuu za kupitishia Wahamiaji Haramu kuingia Tanzania.
Mji wa Taveta Nchini Kenya unaopakana na Wilaya ya ROMBO na Milima ya Upare unatajwa kuwa mojawapo ya Njia kuu za kupitishia Wahamiaji Haramu kuingia Tanzania.
VYANZO VYA MAPATO YA SERIKALI ZA MITAA (HALMASHAURI YA ROMBO)
MAPATO
YA SERIKALI ZA MITAA
Serikali za Mitaa zina Mamlaka ya kukusanya
aina Fulani ya Mapato kutokana na Kodi, levies
na fees. Serikali za Mitaa huweka
Sera zao za Mapato kulingana na mipaka ya Serikali Kuu. Hubakisha Mapato haya
na kuyatumia kama sehemu za Bajeti zao – Mapato
haya sio sehemu ya Mapato ya Serikali Kuu. Kodi, levies, fees na Vyanzo vya Mapato ambavyo Serikali za Mitaa zina
Mamlaka ya kukusanya zimewekwa kwa
mujibu wa Local Government Finances Act
kama ifuatavyo:
A. Taxes on Property
i.
Property rates.
B. Taxes on Goods and Services
- Crop cess (maximum 5% of farm gate price)
- Forest produce cess
C. Taxes on Specific Services
i.
Guest
house levy
D. Business and Professional Licenses
- Commercial fishing license fees
- Intoxicating liquor license fee
- Private health facility license fee
- Taxi license fee
- Plying permit fees
- Other business licenses fees
E. Motor Vehicles, Other Equipment and Ferry Licenses
- Vehicle license fees
- Fishing vessel license fees
F. Other Taxes on the Use of Goods, Permission to Use Goods
- Forest produce license fees
- Building materials extraction license fee
- Hunting licenses fees
- Muzzle loading guns license fees
- Scaffolding / Hoarding permit fees
G. Turnover Taxes
i.
Service
levy
H. Entrepreneurial and Property Income
- Dividends
- Other Domestic Property Income
- Interest
- Land rent
I. Administrative Fees and Charges
- Market stalls / slabs dues
- Magulio fees
- Auction mart fees
- Meat inspection charges
- Land survey service fee
- Building permit fee
- Permit fees for billboards, posters or hoarding
- Tender fee
- Abattoir slaughter service fee
- Artificial insemination service fee
- Livestock dipping service fee
- Livestock market fee
- Fish landing facilities fee
- Fish auction fee
- Health facility user charges
- Clean water service fee
- Refuse collection service fee
- Cesspit emptying service fee
- Clearing of blocked drains service fee
- Revenue from sale of building plans
- Building valuation service fee
- Central bus stand fees
- Sale of seedlings
- Insurance commission service fee
- Revenue from renting of houses
- Revenue from renting of assets
- Parking fees
J. Fines, Penalties and Forfeitures
- Stray animals penalty
- Share of fines imposed by Magistrates Court
- Other fines and penalties
Mamlaka za Serikali za
Mitaa ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya ROMBO
hazipaswi kutoza taxes, levies au fees
ambazo hazipo katika orodha hii.
Monday, 27 August 2012
BIASHARA YA FEDHA HARAMU (MONEY LAUNDERING)
Biashara ya Fedha Haramu (Money
Laundering) ni
Nini?
MAPITIO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA NA UJENZI.
MAPITIO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2011/2012 NA MAKISIO KWA MWAKA 2012/2013 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO SEKTA ZA MAJI NA NA UJENZI.
Chanzo:
Hotuba za Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013.
1.0: SEKTA YA
UJENZI:
MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2011/2012
Miradi inayoendelea ni pamoja na Miradi mikubwa ya barabara katika
mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga yenye jumla ya Tshs
bilioni 328.235.
Wilaya ya Rombo ina Mradi wa barabara ya;
1.
ROMBO MKUU –
TARAKEA (Km 32) wenye thamani ya Tshs bilioni 15.80
2.
Mradi wa barabara ya MARANGU – ROMBO MKUU – KILACHA –
MWIKA (Km 34) Tshs bilioni 25.10
3.
MARANGU –
TARAKEA – KAMWANGA/BOMANGOMBE – SANYA JUU (Km 173) na ARUSHA – MOSHI – HOLILI zimetengewa
Tshs Milioni 7,854.406
4.
Milioni
488.00 Fedha za Ndani zimetengwa kwa ajili ya kulipia sehemu ya malipo
ya mwisho ya Mkandarasi wa barabara ya TARAKEA – ROMBO.
5.
Tshs Milioni 2,146.00 kwa ajili ya kukamilisha Km
6 za lami kwa barabara ya MARANGU – ROMBO MKUU na MWIKA KILACHA (Km 34).
6.
Milioni 2,926.00 zimetengwa kwa ajili ya kuanza
maandalizi ya Ujenzi wa sehemu ya
barabara ya KAMWANGA – SANYA JUU (Km 75)
7.
Milioni 1,366 kuanza ukarabati wa sehemu ya
barabara ya ARUSHA – MOSHI –HOLILI kwa kiwango cha lami.
8.
FEDHA ZA MATENGENEZO NA USIMAMIZI KWA KIPINDI CHA
JULAI 2011- JUNI 2012 KWA MWAKA WA FEDHA 2010/2011 ZILIZOPELEKWA KWENYE HALMASHAURI YA ROMBO NI TSHS 428,210,377
Labels:
Bajeti 2011/2012,
bajeti halmashauri ya wilaya,
Barabara,
Maji,
Rombo,
Ujenzi
Location:
Mkuu, Tanzania
Friday, 24 August 2012
Mramba azidi kumkandamiza Mkapa mahakamani
Thursday, 23 August 2012 20:19 (Chanzo: Gazeti la Mwananchi) |
Mramba aliyaeleza hayo jana wakati akijitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni na kwamba alitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo ili kutekeleza matakwa ya mkataba. Alidai kuwa kifungu cha 4.3.1 kilichopo kwenye mkataba huo ulioingiwa kati ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Alex Stewart Government Business Assayers kinasema malipo yoyote yatakayolipwa na mkataba huo hayatotozwa kodi. “Mimi nilichofanya ni kutekeleza matakwa ya mkataba huu kwa sababu Waziri wa Fedha pekee ndiye mwenye mamlaka ya kutekeleza mkataba huo,” alidai Mramba. |
Wednesday, 22 August 2012
SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012: NINI MAANA YA SENSA?
Sensa ni zoezi la kuhesabu watu wote waliomo nchini,
kujua mgawanyiko wa watu hao katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na
maeneo ya utawala na ukusanyaji wa taarifa nyingine zinazohusiana na watu na
makazi yao.
HISTORIA YA SENSA TANZANIA.
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910.
Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978,
1988 na 2002. Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002,
idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603. Sensa ya 2012 itakuwa Sensa ya tano baada ya uhuru.
LENGO KUU LA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012.
- Kwa ujumla, takwimu za sensa ya watu ni za muhimu sana katika kupanga mipango inayohusiana na uchumi, utawala na huduma mbalimbali zinazohitajika katika kuinua hali ya maisha ya watu kitaifa.
- Takwimu zitokanazo na Sensa uchangia katika uboreshaji wa maisha ya Watanzania kwa kutoa Takwimu sahihi na zinazoendana na wakati kwa ajili ya kutunga sera, kupanga mipango ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma za jamii, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa program mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya watu. Sense zote ni muhimu lakini Sensa ya mwaka 2012 ina umuhimu wake wa kipekee kwa kuwa itatoa viashiria vingi vitakavyotumika katika kutathimini program za MKUKUTA, MKUZA, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa Tanzania Bara na 2020 kwa Tanzania Zanzibar, Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano wa 2011/12-2015/16 na Malengo ya Milenia ifikapo 2025. Viashiria hivi muhimu nipamoja na idadi ya watu ki makazi, ukubwa wa nguvu kazi, idadi ya vifo na vifo vinavyotokana na uzazi, wastani wa umri wa kuishi wa Mtanzania, viwango vya uzazi, idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika na idadi ya watoto walioandikishwa shule. Viashiria vingine ni pamoja na idadi ya kaya zinazoshujishughulusha na kilimo, ufugaji na uvuvi.
Labels:
Sensa 2012,
Sensa Tanzania,
Tanzania
Location:
Tanzania
Saturday, 4 August 2012
Lengo
DIRA
- Kuwa na Mtandao wa Wakazi wa Rombo unaolenga kuongoza, kushiriki, kushawishi maamuzi na Maendeleo ya Rombo kwenye nyanja mbalimbali.
DHANA
- Kuwa na Mtandao mpana wenye kujumuisha Wananchi wa Kada zote utakaokuwa na ushawishi katika Sera na Mipango ya Maendeleo ya Wilaya ya Rombo.
- To reveal Rombo to ideas, analyses and Challenges toward Sustainable development and Reform
- Expose, Debate and Assess Rombo's growth potentials and limitations.
- To provide a forum/platform for discussion for a consistent and dedicated development and reform agenda towards a prosperous, Democratic and a Human right conscious Rombo District.
- Kutafuta, kujadili, kushawishi na Kusambaza Habari zinazohusu wilaya ya Rombo.
Subscribe to:
Posts (Atom)